Jumuiya ya IGAD yataka kuhitimishwa mgogoro wa wakimbizi Somalia.

Jumuiya ya IGAD yataka kuhitimishwa mgogoro wa wakimbizi SomaliaJumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imesisitiza tena uungaji mkono wake wenye lengo la kuhitimisha mgogoro wa wakimbizi nchini Somalia.

Mawaziri wa Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD waliahidi jana katika mkutano wao mjini Nairobi Kenya kwamba, watatumia suhula zote zilizopo ili kuhakikisha kwamba, mgogoro wa wakimbizi nchini Somalia unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imesisitiza kwamba, kuandaliwa vyanzo vya fedha, ushiriki wa pamoja na kuweko irada ya kisiasa kwamba, ndio njia pekee ya kupunguza matatizo yanayowakabili wakimbizi wapatao laki tisa wa Somalia.
Mkutano huo wa Nairobi Kenya pamoja na mambo mengine umekuwa na lengo la kuangalia upya hatua iliyopigwa katika kutekeleza makubaliano ya kieneo yanayohusiana na suala zima la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa wakimbizi Somalia.
Zaidi ya Wasomali milioni mbili wametawanyika huku na kule duniani kutokana na moja na migogoro ya muda mrefu sana ulimwenguni na wengi wamepata hifadhi katika nchi jirani za Kenya, Ethiopia, Yemen, Uganda na Djibouti.
Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD  ambayo inaundwa na nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda na imekuwa mstari wa mbele katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo.  
chanzo:parstoday.

Comments