Taarifa iliyotolewa jana Alkhamisi na kituo hicho imefichua kuwa, kesi 67 za watoto wa Kipalestina kukamatwa na kutiwa kizuzini na maafisa usalama wa utawala katili wa Israel zimerekodiwa mwezi uliopia wa Februari pekee.
Taarifa ya PPS imesema kuwa, tayari kuna zaidi ya watoto wadogo 180 walio chini ya umri wa miaka 13 wanaozuiliwa katika gereza la kuogofya la Ofer, karibu na mji wa Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Loai Mansi, mwakilishi wa wafungwa watoto katika gereza hilo la Ofer amesema makumi ya watoto wanaozuiliwa hapo wanakabiliwa na mateso na unyanyasaji wa kupindukia kila uchao kutoka maafisa usalama wa Israel.
Ameongeza kuwa, watoto wadogo karibu 170 wanazuiliwa katika jela za Megiddo na Hasharon chini ya mazingira magumu yasiyo ya ubinadamu.
Kwa mujibu wa takwimu za Kundi la Haki za Binadamu la adh-Dhamir la Palestina, takribani Wapalestina 7,000 wakiwemo mamia ya watoto wadogo wanashikiliwa katika magereza ya utawala haramu wa Israel huku wakiwa katika mazingira mabaya.
chanzo:parstoday.
Comments