Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika
Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
Mwengine aliyeapishwa ni Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa
Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir
Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa
Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Katika maelezo yao viongozi hao mara baada ya kuapishwa waliahidi
kutekeleza majukumu yao kwa mashirikiano ya pamoja kati yao na viongozi
wengine wote wa Serikali wakiwemo wale wa Wizara zao pamoja na Ofisi
watakazoziongoza.
chanzo:Ikulu Zanzibar
Comments