Chuo Basra, Miembeni City zatota Ligi Kuu.

MZUNGUKO wa 20 wa Ligi Kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba, umeanza kutimia vumbi lake katika uwanja wa Gomabani majira ya saa 8:00 za mchana kwa timu ya Wawi star kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chuo Basra.

Mchezo huo uliopigwa huku kijua kikali kikiwaka uwanjani hapo, timu hizo zimeshuka uwanjani Wawi ikiwa na pointi 22 ikishika nafasi ya 10, huku Chuo Basra ikiwa na pointi 17 ikishika nafasi ya 13 katika ligi hiyo.

Timu hizo zilikianza kipindi cha kwanza kwa kasi kubwa huku kila timu ikihitaji ushindi uwanjani hapo, kila timu ikikosa mabao ya wazi baada ya washambuliaji wa timu hizo kutokuwa makini.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa, kila timu ikifanya mabadiliko ya wachezaji wao, ili kuweza kupata bao la kuongoza , mabadiliko hayo yaliweza kuwasaidia Wawi Star dakika ya 59 kwa kuandika bao lililofungwa na Sadam Maulidi.

Comments