Mwanamuziki
wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka na kuweka wazi kilicho
sababisha kuwepo kwa ugomvi kati yake na msanii mwenzake Ney wa Mitego.
Sakata
hilo lilianza baada ya Nay wa Mitego kumchana Barakah kwenye wimbo wake
uitwao ‘Moto’ aliouachia mwaka jana mwezi Julai ambapo kwenye wimbo
huo Nay aliimba; Itafika hatua tuchangishane elfu hamsini tuwarudishe wadogo zetu Mwanza akamtaja Barakah the Prince.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na Jembe Fm, Barakah amefunguka na kusema kisa cha
Nay kumuimba vile ni baada ya yeye kumchana na kumwambia kipaji chake
cha kurap ni kidogo:
"Nay
wa Mitego mimi nilishawahi kumwambia studio kwake kwamba wewe sio rapa
mkali .Nilitoka studio nikamkuta [Nay] anadiss kuhusu Godzilla, mimi
nikamwangalia nikamwambia huyu jamaa mbona kipaji chake kidogo sana.
"Ujue
Godzilla ni rapa sasa wewe Nay Wamitego unarap kitu gani? Haumfikii
Godzilla hata kidogo, wewe ni msanii unaunga unga. Hapo ndipo
alipopaniki akaamua kwenda kuniimba, siwezi kumjibu mtu ambaye hana
kipaji”.
Comments