Awali Michael Dodman, balozi wa Marekani nchini Mauritania alikuwa amehudhuria sherehe katika kituo kidogo cha mafunzo ya lugha ya Kingereza katika Taasisi ya Elimu ya Juu ya Utalii na Utafiti ya Kiislamu mjini Nouakchott.
Hata hivyo kelele za malalamiko zilizofanywa na wanafunzi waliokuwa wakilaani hatua ya Rais Trump ya kuutaja mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala bandia wa Kizayuni, zilimfanya Dodman, kuondoka katika sherehe hizo haraka.
Kadhalika kelele hizo za wanafunzi zililaani uamuzi wa serikali ya Marekani wa kutaka kuhamisha ubalozi wa nchi hiyo kutoka Tel Aviv na kuupeleka Baitul-Muqaddas.
Itakumbukkwa kuwa, tarehe sita Disemba mwaka jana, Rais Donald Trump wa Marekani na licha ya kuwepo upinzani mkubwa kieneo na kimataifa, aliutangaza mji huo wa Quds kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, suala ambalo lilikabiliwa na radiamali kali kutoka duniani.
chanzo:parstoday.
Comments