
Hakimu Judicaster Nthuku amesema kuwa ushahidi
unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alifanya vitendo hivyo vya ubakaji, na
ripoti ya daktari kuthibitisha hilo huku akimuambukiza ugonjwa wa zinaa
aina ya ngono.
Mahakama imeelezea kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ni rafiki wa karibu
wa familia ya binti huyo, ambapo siku ya tukio alimuita na kumtaka
kumsaidia kazi za nyumbani, na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha
ukatili na udhalilishaji.
Sambamba na hilo mwanaume mwengine mwenye umri wa miaka 74
aliyetambulika kwa jina la Kipngeno arap Bor katika eneo la Subukia
nchini Kenya huko huko Nakuru, amehukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la
kumbaka mjukuu wake, ambaye mashahidi walimkuta akifanya tendo hilo
baada ya kusikia kelele za binti huyo akilia na kuomba msaada.
Chanzo: zanzibar24.
Comments