Tovuti ya habari ya Garowe imeripoti kuwa, siku ya Ijumaa, gari lililokuwa limesheheni mada za milipuko liliingia katika kambi ya jeshi wilayani Afgoye, eneo la Lower Shabelle, yapata kilomita 30 magharibi mwa mji mkuu Mogadishu na kuripuka.
Captain Ibrahim Hassan, afisa wa polisi katika eneo hilo amethibitisha kutokea hujuma hiyo na kuongeza kuwa askari 6 wa serikali ya Somalia waliuawa, mbali na raia kadhaa.
Gaston Sindimwo, Makamu wa Rais wa Burundi amesema askari watano wa nchi hiyo waliokuwa wakihudumu chini ya mwavuli wa Amisom waliuawa katika shambulizi la al-Shabaab katika eneo la Bal'ad, eneo la Shabelle ya Kati Ijumaa.
Hata hivyo kundi hilo lenye mfungamano na mtandao wa al-Qaeda limedai kuua watu 80 wakiwemo maafisa usalama wa ndani na nje ya nchi katika hujuma zake hizo.
Hii ni katika hali ambayo, Alkhamisi iliyopita katika mkutano wa wakuu wa majeshi na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizochangia askari wa Amisom huko Kampala Uganda, kikosi hicho kilitangaza kuwa kimefanikiwa kukomboa asilimia 80 ya maeneo ambayo yalikuwa kwenye makucha ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab.
chanzo:parstoday.
Comments