Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Laafey huko kaskazini mwa Kenya, Eric Oronyi amesema shambulizi hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo, ambapo wanamgambo hao wamevamia kituo cha polisi wa kawaida na wa utawala katika mji wa Fino.
Amesema wavamizi hao kati ya 70 hadi 100 mbali na kutekeleza mauaji hayo, kadhalika wameng'oa mlingoti wa shirika moja la simu za rununu na kulemaza mawasiliano.
Mwezi uliopita, maafisa wengine watano wa polisi ya Kenya waliuawa baada ya wanachama wa al-Shabaab kushambulia msafara wa magari ya maafisa usalama katika barabara ya Elwak-Kotulo katika kaunti hiyo hiyo ya Mandera.
Kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye makao yake Somalia mara kwa mara hutekeleza mashambulizi ndani ya ardhi ya Kenya kuishinikiza serikali ya nchi hiyo iondoe wanajeshi wake wanaohudumu katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika Somalia, AMISOM.
chanzo:parstoday.
Comments