Wanigeria waendeleza maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaki aachiliwe huru..

Wanigeria waendeleza maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaki aachiliwe huru.Wanachama wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria wanaendeleza maandamano ya amani ya kutaka aachiliwe huru kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Taarifa zinasema kuwa wikendi hii maandamano yameendelea katika maeneo mbali mbali ya Nigeria hasa katika mji wa Zaria jimboni kaduna ambapo waandamanaji wametaka Sheikh Zazkay na mke wake waachiliwe huru mara moja.
Itakumbukwa kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky alitiwa nguvuni na jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 baada ya kuvamia makazi yake katika mji wa Zaria jimboni Kaduna na kufanya mauaji ya umati dhidi ya Waislamu. 
Taarifa zinasema mamia ya Waislamu waliuawa shahidi katika hujuma hiyo wakiwemo watoto watatu wa Sheikh Zakzaky.
Hata hivyo licha ya mahakama kutoa hukumu ya kutaka kuachiwa huru mwanazuoni huyo, bado vyombo vya usalama vya Nigeria vinaendelea kumshikilia katika korokoro isiyojulikana huku ripoti zikifichua kwamba hali yake ya kiafya ni mbaya.
chanzo:parstoday

Comments