Wananchi watakiwa kutumia lugha ya kiswahili.

Image result for Jumuiya ya kukuza na  kuendeleza Lugha ya  Kiswahili ZanzibarJumuiya ya kukuza na  kuendeleza Lugha ya  Kiswahili Zanzibar  [JUWAKIZA] wamewataka  wananchi kujiunga  katika jumuiya hiyo ili kuweza kutumia lugha  kwa ufasaha.

Yameelezwa hayo na Katibu wa Jumuiya hiyo Dr  Omar Abdallah Adam kuwa lugha ya kiswahil ni fursa yetu wazanzibar kujua  umuhimu wake    kusoma na kuandika, kutumia kiswahil inavotakiwa kwani lugha yetu ni rasilimali ya taifa.

Ameongeza kusema kuwa wana mbinu mbali mbali wanazozitumia ili kukuza na kukiendeleza lugha ikiwemo kutoa elim maskulin na vyuon, kueka vipindi ndani ya vyombo vya habar,kutumia  katika mitandao ya kijamii,kutunga mashairi na tenzi.

Aidha ametoa wito kwa wanzanzibar hususani wenye kiwango cha masta na degree kujiunga na jumuiya kwani lugha inayotumika ni taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake mwanachama wa Jumuiya hiyo Mwanakombo Ali amesema tangu ajiunge na jumuiya hiyo amefaidika kwa kukionesha kipaji chake kwa kutunga na kusoma mashairi na utenzi kiufasaha.

Comments