
Akizungumza na zanzibar24 baada ya tukio la ukataji miti kinyume na sheria lililofanywa Fuoni Uwandani Afisa Misitu Wilaya ya Magharib B Shadhil Shauri Suleiman amesema wananchi wamekuwa wakikata misitu kinyume na sheria na kusababisha uharibifu wa Mazingira.
Amesema licha ya wananchi kupewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira lakini baadhi ya watoto wa viongozi wamekuwa hawaifanyii kazi elimu hiyo jambo ambalo linachangia kupotea kwa miti ya asili hapa Zanzibar.
‘’Hii sehemu inavyosemekana ni ya familia ya Marehemu Abod Jumbe na limekatwa miti kinyume na sheria lakini tulilizuia mwanazo lisikatwe lakini waliendelea na ukataji miti jambo ambali linaleta picha mbaya kwa wananchi na kusema watoto wa viongozi wanakiuka sheria zilizowekwa’’
Aidha ametowa kwa Viongozi na wananchi kuendelea kufuata sheria za taratibu za misitu zilizowekwa ili kujiepusha na uharibifu wa mazingira unaoharibu haiba ya Nchi.
Kwa uapande wake Sheha wa Shehia ya Fuoni Uwandani Juma Mussa Juma amesema amesikitishwa na tukio hilo ambalo limeenda kinyume na taratibu za Ukataji miti misitu licha ya kuwa walikubaliana kufata sheria za ukataji wa miti.
“walikuja kutoa taarifa kuwa wanahitaji kusafisha shamba lao lakini walikata miti kinyume na utaratibu na niliwambia wafate utaratibu na walinifata tena kutaka barua ya kwenda kutafuta kibali nimewaandikia lakini walishindwa kuwenda sehemu husika ili kupata utaratibu unaofaa’’ alisema Sheha
Kwa upande wake Msaidi wa Afisa Mkuu wa Misitu na Mali zisizorejesheka Zanzibar Makame kitwana Makame aliefika Shambani hapo kuangalia uharibifu huo amesema si vyema kwa wananchi kuendelea kuchukuwa hatua mikononi mwao jambo ambalo linachangia uvunjifu wa sheria.
Amesema seikali hatamuonea muhali na haitamvumilia mwananchi yoyote atakafanya matukio ya uvunjifu wa sheria ikiwemo kukata miti ya jambo ambalo linachangia kuengezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia Nchi zilizoenea kwa kasi katika maazi ya Wananchi.
‘’ si suala la busara kwa watoto wa viongozi kujichukulia hatua mikononi mwao na kuweka zana kuwa hakuna uwezekano wa kuchukuliwa hatua ukweli ni kwamba unapopanda miti cha kwako ni matunda na kivuli tuu ukitaka kukata lazima ufate taratibu’’
Zaidi ya miti aina ya Mishelisheli 17na mitofaaa 5 pamoja na misufii imekatwa katika eneo hilo la eka tatu kinyume na sheria na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
chanzo:Zanzibar24.
Comments