Wanamapinduzi wa Bahrain wasisitiza kuhitimishwa enzi za utawala uliooza wa Aal Khalifa.

Wanamapinduzi wa Bahrain wasisitiza kuhitimishwa enzi za utawala uliooza wa Aal KhalifaKiongozi mmoja wa harakati ya Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14 ya Bahrain amesema: Wanamapinduzi watapinga mpango wowote ule utakaolenga kuubakisha madarakani utawala wa Aal Khalifa.

Sambamba na kuashiria haki ya wananchi wa nchi hiyo wanaowajibika, ya kujiamulia hatima yao ya kisiasa, Dhiyaa al-Bahrani amesisitiza kuwa harakati halali na za haki za mwaka wa saba wa Mapinduzi ya wananchi hao zitaendelea katika mwaka huu kwa anuani ya "Wenye Kuendelea Kubaki."
Al- Bahrani amesema, ujumbe wa Mapinduzi ya Februari 14 nchini Bahrain ni istiqama na muqawama katika harakati ya kusimamisha fumo wa kidemokrasia nchini na akaongezea kwa kusema: watu wa nchi hii wanataka mfumo utakaotawala ardhi ya nchi hii kwa uadilifu, usawa na wenye mamlaka kamili ya kujitawala. 
Ni miaka saba imepita tangu lilipoanza vuguvugu la mapinduzi ya wananchi wa Bahrain yaliyopewa jina la "Mapinduzi ya Lulu;" mapinduzi ambayo watu wake wameendelea kuwa ngangari na kusimama imara licha ya kukabiliwa na siasa na hatua kandamizi za utawala Aal Khalifa.
Tangu Februari 11 mwaka 2011, Bahrain inashuhudia wimbi la mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala  wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa. 
Wananchi wa Bahrain wanataka uhuru wa kisiasa, kutekelezwa uadilifu, kuondolewa ubaguzi na upendeleo na kuongozwa nchi yao na serikali iliyochaguliwa na wananchi wenyewe.
chanzo:parstoday.

Comments