Kwa mujibu wa shirika hilo, wanajeshi katili na walowezi wa Kizayuni wamewashambulia vijana wa Kipalestina katika mji wa Ariha wa mashariki mwa Ukingo wa Magharibi na kijiji cha Kufr Aqab kaskazini mwa mji wa Quds.
Shirika hilo la misaada ya kibinadamu la Palestina limeongeza kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni limewashambulia kwa risasi za kivita vijana wa Palestina pamoja na gesi za sumu.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa binti mmoja wa Kipalestina amejeruhiwa vibaya kwa risasi za wanajeshi wa Israel katika kijiji cha Kufr Aqab.
Jumamosi usiku, mtandao wa Intifadha ya Palestina uliripoti kuwa mwezi uliopita wa Januari, Wapalestina 9 wameuawa shahidi na wengine 203 kujeruhiwa na wanajeshi makatili wa Israel.
Mauaji dhidi ya Wapalestina yameongezeka sana hivi sasa baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kudai kuwa mji wa Quds ambao una Kibla cha Kwanza cha Waislamu eti ni mji mkuu wa utawala pandikizi wa Kizayuni.
Licha ya kulaaniwa na kulalamikiwa vikali kote ulimwengu, lakini tarehe 6 Disemba 2017, Donald Trump alifanya kiburi ya kutangaza rasmi kuwa anaitambua Quds kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.
Uamuzi huo wa Trump ulipingwa kote duniani bali na hata Umoja wa Mataifa ambao tarehe 21 Disemba 2017 ulipitisha azimio muhimu na kutangaza rasmi kwamba Quds ni mji mkuu wa Palestina na kamwe hauwezi kukubaliana na uamuzi huo wa Trump.
Comments