Sisitizo hilo limetolewa na shakhsia hao
wawili wakati walipoonana na kufanya mazungumzo katika mji mkuu wa
Lebanon, Beirut, jana Jumatano.
Wamegusia namna Israel na watu wenye
fikra za Kizayuni kama rais wa Marekani, Donald Trump wanavyofanya njama
dhidi ya Palestina na kuutaka umma wa Kiislamu kuwa macho na Waislamu
kubakia katika njia sahihi ya kukabiliana na maadui wao wa pamoja badala
ya kuzozana wao kwa wao.
Imam wa Sala ya Ijumaa ya Beirut pia
amesisitiza kwamba, umoja na mshikamano wa Kiislamu ndiyo stratijia
pekee ya kuweza kuwasaidia Wapalestina na kuunga mkono muqawama.
Amesema, Waislamu kote ulimwengu wanapaswa kusimama kidete kupambana na
njama za rais wa Marekani Donald Trump za kutaka kuifuta kabisa kadhia
ya Palestina kupitia kuitangaza Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala wa
Kizayuni wa Israel.
Kwa upande wake, Sheikh Maher Mahmoud,
Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amesema, umoja huo
daima umekuwa ukifanya juhudi za kulinda umoja wa Lebanon, wa Waarabu na
wa Waislamu sambamba na kuulinda muqawama mbele ya adui Mzayuni.
chanzo:parstoday..
Comments