Sherehe hizo zimeanza rasmi leo
Alkhamisi saa 3:27 asubuhi kwa saa za hapa Iran kwa wimbi kubwa la
wananchi kukusanyika katika Uwanja wa Ndege wa Mehrabad hapa Tehran
alipofikia Imam Khomeini kutokea Ufaransa mwaka 1979.
Imam Khomeini alirejea nchini Iran
Februari 1, 1979, na kuongoza moja kwa moja Mapinduzi ya Kiislamu akiwa
humu humu nchini. Ushindi wa mapinduzi hayo matukufu ulipatikana siku
kumi tangu baada ya kurejea nchini Imam Khomeini MA.
Hivyo Februari 1
kila mwaka ni siku ya kuanza sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
nchini Iran.
Imam Khomeini alipitisha zaidi ya miaka
14 nje ya nchi baada ya watawala wa wakati huo wa Iran kumfukuza nchini.
Miaka mingi aliipitisha mjini Najaf Iraq. Aliishi pia Uturuki na
Ufaransa kabla ya kurejea Iran na kuongoza moja kwa moja Mapinduzi ya
Kiislamu.
Siku hiyo ya Februari 1, 1979 mamilioni
ya watu walimiminika katika mitaa na barabara za mji mkuu Tehran
kumpokea kiongozi wao. Sherehe hizi hufikia kileleni Februari 11 siku ya
ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu, kila mwaka.
Comments