
Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Salama Aboud Talib,
aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakati akitoa ufafanuzi
kufuatia kujitokeza kwa tatizo la uhaba wa nishati hiyo katika kipindi
cha wiki moja.
Alisema faini iliyotozwa kwa vituo hivyo inatokana na kuficha mafuta na kuyauza kwa bei ya ulanguzi.
Akifafanua zaidi alisema ni kweli ulikuwepo uhaba wa mafuta katika
kipindi cha wiki moja ambao ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya
mafuta ya Unite Petroleum, kukabiliwa na uhaba wa mafuta katika hifadhi
yake.
Alisema upungufu huo ulichangiwa na kuchelewa kwa upakuzi wa mafuta
katika Bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa sasa imeweka utaratibu mpya.
Hata hivyo, Talib alisema serikali imeziona changamoto mbali mbali
zinazojitokeza katika kutoa huduma ya nishati ya mafuta kupitia Mamlaka
ya Udhibiti wa Nishati ya Mafuta Zanzibar (Zura).
Aidha, aliwatoa hofu wananchi kuwa kuna mafuta ya kutosha kwa
matumizi mbali mbali ya wananchi wa Zanzibar huku akitoa onyo kali kwa
kampuni zilizopewa leseni ya kutoa huduma hiyo kuacha kutumia mwanya wa
upungufu wa mafuta na kuongeza bei kwa njia ya ulanguzi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia Kamati ya Habari na
Utalii, walisikitishwa na tatizo la kuwpo kwa uhaba wa nishati ya mafuta
mara kwa mara ambalo ni moja ya kikwazo cha kuyumba kwa biashara ya
sekta ya utalii.
chanzo: Zanzibar24.
Comments