Mkurugenzi wa UNICEF katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Kahirat Kabbalari amesema kuwa, watoto hao wameuawa katika mapigano yaliyotokea kwenye nchi za Iraq, Libya, Palestina, Syria na Yemen.
Kabbalari ameongeza kuwa, kuendelea kuuawa na kujeruhiwa watoto ni jambo lisilokubalika na kwamba watoto hao wasio na hatia wanalipa gharama kubwa zinazosababishwa na vita na mapigano.
Mkurugenzi wa UNICEF Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amesema kuwa, mamilioni ya watoto wanaishi katika hali mbaya na wamekuwa wakitiwa nguvuni, kutumiwa vibaya na kunyimwa haki zao za msingi.
Makundi ya kigaidi kama Daesh ambayo yameanzishwa na kufadhiliwa na Saudi Arabia, Israel na Marekani, na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen yanahatarisha maisha ya mamilioni ya watoto katika nchi mbalimbali.
chanzo:parstoday.
Comments