
Lissu ambaye pia ni rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS)
anayeendelea na matibabu ya viungo katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha
Leuven nchini Ubelgiji alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi.
“Mie naendelea vizuri na kwa sasa ninaweza kusimama kidogo tu. Sijaanza kutembea bila magongo,” alisema.
Kuhusu hali ya mguu wa kulia ambao uliathirika zaidi na risasi alizoshambuliwa Septemba 7, 2017 mjini Dodoma, alisema: “Bado sio salama sana na unahitaji kufanyiwa kazi ya kitabibu zaidi.”
Awali, Lissu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa jamii wa Instagram
aliandika ujumbe wa kumshukuru Mbunge wa Tandahimba (CUF), Ahmad Katani
aliyemtembelea Ubelgiji na picha ya wawili hao ilianza kusambaa juzi
usiku mitandaoni ikiwaonyeasha wakiwa na nyuso za furaha.
Lissu alimshukuru mbunge huyo kwa kumtembelea huku akieleza kuwa ni
miongoni mwa wabunge waliompeleka Nairobi nchini Kenya akitokea
Hospitali ya Rufaa ya Dodoma alipopelekwa baada ya kushambuliwa.
“Katani alikuwa kwenye msafara wa wabunge walionipeleka
Nairobi, Kenya mara baada ya jaribio la mauaji la Septemba 7 na alikaa
Nairobi kwa siku nne. Nimefarijika sana na ugeni huu wa ndugu yangu na
kaka yangu Katani,” alisema mbunge huyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments