SMZ: Ofisi ya muft haina malaka ya kusikiliza kesi za migogoro za usimamizi wa mali za taasisi za dini.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Ofisi ya Mufti mkuu haina Mamlaka ya kusikiliza Kesi za Migogoro ya Usimamizi wa Mali za Taasisi za Dini na kuzitolea hukumu badala yake kesi zitaendele kupelekwa katika mahkama kuu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Katiba, Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kushoto akizungumza na Viongozi wa Ofisi ya Mufti Zanzibar nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mara baada ya kusomwa muhtasari wa Ripoti ya Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani, Naibu Waziri wa Nchi OR Katiba na sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis  Juma Mwalimu amesema Ofisi ya Mufti itaendelea na majukumu yake ya kutoa suluhu ya kesi na sikukutoa hukumu za Migogoro ya Usimamizi wa Mali za dini.
Amesema licha ya Ofisi hiyo kutoa suluhu lakini Baadhi ya Wananchi wanakimbilia Mahakamani kutokana na kutoridhika kwa suluhu hiyo ili waweze kunufaika na haki zao za msingi.
Amesema kwa kipindi cha Mwaka 2015 hadi Disemba 2017 jumala ya kesi 29 za usimamizi wa mali za Miskiti ambapo kwa upande wa kesi za mirathi ni 260 zimefunguliwa katika mahkama kuu.
chanzo:Zanzibar24.

Comments