Serikali
imeamua kusitisha hati za kusafiria za viongozi kadhaa wa ngazi ya juu
na wanasiasa wafuasi wa muungano wa upinzani wa Nasa ikiwemo ya gavana
wa Mombasa, Hassan Joho.
Mbali
ya Joho, wanasiasa wengine waliositishiwa hati zao za kusafiria ni
seneta wa Siaya, James Orengo na seneta wa zamani wa Machakos, Johnson
Muthama.
Mpangaji
mkuu wa mikakati wa muungano huo, David Ndii pamoja na mfanyabiashara
Jimi Wanjigi pia hawakuachwa katika mkumbo huo wa serikali kuzidisha
kibano kwa wanasiasa wa upinzani baada ya hatua yao ya "kumuapisha”
mgombea wao wa urais katika uchaguzi wa mwaka jana Raila Odinga kuwa
"rais wa watu" ikiwa ni ishara ya kutotii serikali.
Katika
barua waliyopelekewa viongozi hao wanaodaiwa kufikia 15, Mkurugenzi wa
Uhamiaji, Gordon Kihalang'wa alisema kusitishwa kwa hati hizo
kumefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Wananchi na Uhamiaji ya mwaka 2011
inayotoa sababu za kusimamishwa.
Akizungumza
na Daily Nation Jumanne, Muthama alisema viongozi kutoka idara ya
uhamiaji walitoa barua hiyo ya kumjulisha kuhusu hatua ya kusitishiwa
hati ya kusafiria kuanzia saa 7:00.
"Tunaona
udikteta ukijitengeneza. Hawaheshimu sheria kwa sababu hili ni
shambulio dhidi ya Sheria ya Haki ambayo haiwezi kuachanishwa," alisema.
Seneta
huyo wa zamani ambaye pia ni kiongozi wa ngazi ya juu wa upinzani
alisikitishwa kwamba njia zisizofaa zinazotumika kwake tayari
zimemvuruga.
"Ilikuwa
nimsindikize binti yangu Uingereza leo (Jumanne) saa 10:00 alasiri
lakini sasa siwezi. Hii ni njia hatari ambayo serikali imechagua na
lazima isitishwe," alisema.
Kinara
wa Nasa, Kalonzo Musyoka ameelezea kusimamishwa kwa hati za kusafiria
kwa viongozi wa juu wa Nasa na kufungwa kwa vyombo vya habari kuwa ni
sifa za serikali yenye hofu.
"Hofu
ambayo imeingia kwenye utawala huu inaelezea yote. Wanaziba uhuru wa
vyombo vya habari kwa sababu hawataki ukweli, na sasa wameamua kuzuia
watu kusafiri. Lakini kwa nini wana hofu? Kama wako imara kama
wanavyosema, hofu ya nini?" Aliuliza Musyoka alipokuwa kwenye ofisi za
makao makuu ya chama chake cha Wiper jana.
chanzo:Mpekuzi.
Comments