Serikali yaombwa kuwaangalia upya watu wenye ulemavu Zanzibar.

Mkurugenzi  Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar Asia Abuu Salami  ameiomba serikali  na Taasisi mbalimbali za maendeleo nchini, kuwapa kipaumbele zaidi watu wenye ulemavu na wasiojiweza pindi zinapotokea   fursa za kimaendeleo kwa wananchi.

Akizungumza na Zanzibar24 amesema  ni vyema Watu wenye ulemavu  kupewa haki sawa za kimaendeleo na watu wengine wasokuwa na ulemavu ili kila mmoja wao ajihisi huru kama wengine kwani nao wakiwezeshwa wanaweza.

Aidha Mkurugenzi  Asya  amebainisha kuwa  bado watu wenye ulemavu  wanakabiliwa na changamoto  nyingi katika jamiii ikiwemo ukosefu wa vifaa wanavyotumia kwa shughuli zao za kila siku kama vigari vya kutembelea, Fimbo, Miwani na kadhalika.

Hivyo muda imewadia kwa taasisi za maendeleo  na serikali  kusimama kidete kuwaondolea usumbufu Wenye Ulemavu na Wasiojiweza nchini.

chanzo: Zanzibar24.

Comments