Rais wa Misri akosolewa vikali kufuatia kufichuliwa ushirikiano wake wa siri na utawala wa Kizayuni.
Vyama vya kisiasa vya upinzani na wanasiasa nchini Misri wamemkosoa pakubwa Rais Abdul Fattah al Sisi kufuatia kufichuliwa ushirikiano wa siri na wa nyuma ya pazia wa serikali ya Cairo na utawala ghasibu wa Kizayuni.
Imebainika kuwa kufuatia kuwepo ushirikiano huo wa siri, Misri iliuruhusu utawala ghasibu wa Israel kutumia jangwa la Sinai zaidi ya mara mia kutelekeza mashambulizi ya anga kwa madai ya kuwashambulia magaidi.
Ndege za Israel zisizo na rubani (droni) zimekuwa zikiendesha kisirisiri mashambulizi katika ardhi ya Misri tangu miaka miwili iliyopita; na kufuatia kujiri mashambulio hayo, waandishi habari wamepigwa marufuku kuingia katika Peninsula ya Sinai.
Wanasiasa na wanaharakati wa sekta ya uhalifu wa mitandaoni wamemkosoa pakubwa Rais al Sisi kufuatia kufichuliwa ripoti hiyo.
Wanasiasa na wanaharakati hao wa Misri wanaamini kuwa utawala ghasibu wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu unataka kulikalia tena kwa mabavu eneo la Sinai baada ya kujipenyeza katika eneo hilo na kuwafukuza wakazi wa eneo hilo ili kufanikisha hatua zake za kujitanua.
Comments