
Infantino atakuwa hapa nchini kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka wa
FIFA unaotarajiwa kuanza leo Februari 22 katika ukumbi wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere huku ukitegemewa kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa
Shirikisho hilo.
Baada ya kuwa hapa nchini, Infantino ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.
Mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali
ikiwemo kujadili Maendeleo ya Soka la Wanawake, Maendeleo ya Soka la
Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele
mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.
Rais wa FIFA alimhakikishia Waziri Mwakyembe ushirikiano katika
masuala mbalimbali ya mpira wa miguu. Aidha, Rais wa Fifa alisema
chaguo la kufanyia mkutano huo Tanzania limetokana na maendeleo ya kasi
ya tasnia ya mpira wa miguu na weledi wa viongozi wa TFF waliopo
madarakani.
Aidha Rais wa FIFA, Gianni Infantino amemuambia Waziri Mwakyembe kuwa
FIFA ni Shirikisho lililo la kweli na lenye uwazi na ndiyo maana wapo
Tanzania kwakuwa ni sehemu ya ulimwengu ambao soka linachezwa nakuja
nchi hii kuna mchezaji bora wa Afrika anaechezea KRC Genk akitokea hapa
ambaye ni Mbwana Samatta.
Infantino anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.
Comments