Ripoti zinasema kuwa wafanya mashambulizi kadhaa wameuawa pia katika mapigano yaliyojiri huko Talataye kaskazini mwa Mali.
Mji wa Talataye unapatikana kaskazini mashariki mwa Mali ukiwa na jamii ya watu elfu 14.
Kuzidi kuwa mbaya hali ya usalama huko Mali ni jambo linalozidisha hali ya wasiwasi kwa kuzingatia kuwa makundi yanye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida yamekuwa yakishadidisha mashambulizi makali dhidi ya vikosi vya ndani na nje huko Mali.
Wanamgambo wenye silaha katika mji wa Talataye kwa kawaida hulishambulia kundi la Azawad linaloundwa na watu wa kabila la Tuareg wanaoishi jangwani ambao wanawahesabu kuwa na mahusiano ya karibu na kundi moja linalobeba silaha lenye mfungamano na serikali ya Bamako.
Hayo yameelezwa na afisa mmoja katika mji huo.
Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa mwezi Januari uliopita wanajeshi 14 wa Mali waliuliwa na 18 kujeruhiwa katika shambulio la wanamgambo dhidi ya kambi ya vikosi hivyo huko kaskazini mwa Mali.
chanzo:parstoday.
Comments