Na Lydia Churi-Mahakama ya Tanzania
Viongozi
wanaohusika na Oparesheni za kuzuia uhalifu wameshauriwa kufuata na
kuzingatia sheria inayoongoza namna ya ukusanyaji wa ushahidi ili
kuepuka kuharibu ushahidi kabla haujawasilishwa Mahakamani na kupelekea
kesi nyingi kuharibika kwa kukosa ushahidi au Mahakama kushindwa kutoa
hukumu zinazoendana na kosa husika.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameyasema hayo wakati
akizungumza na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uyui
alipomtembelea Mkuu wa wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake
inayoendelea Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
Akitolea
mfano wa Oparesheni za uteketezaji wa dawa za kulevya yakiwemo mashamba
ya bangi, Jaji Mkuu amesema ushahidi kuteketezwa bila ya kufuata
utaratibu huathiri mienendo ya kesi Mahakamani.
Akizungumzia
suala la Maadili ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amewaomba Wakuu wa mikoa
pamoja na Wakuu wa wilaya ambao anawatambua kama walezi wa Mahakama
kushirikiana kwa karibu zaidi na Mahakama ili kuhakikisha wanawahudumia
wananchi ipasavyo katika suala zima la utoaji wa Haki.
Kuhusu
kusogeza huduma za kimahakama karibu Zaidi na wananchi, Jaji Mkuu
amesema Mahakama kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inao Mpango wa
kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kuwafikia wananchi
walio mbali na huduma za kimahakama hasa katika wilaya ya Uyui mkoani
Tabora
Naye
Mkuu wa wilaya ya Tabora na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Uyui, Queen Mlozi
alimweleza Jaji Mkuu kuwa kwa namna wilaya ya Uyui ilivyokaa
kijiografia, wananchi hulazimika kufuata huduma za kimahakama umbali wa
Zaidi ya kilometa 150 katoka Loya kwenda Kigwa mkoani Tabora.
Awali
akiwa wilaya ya Urambo, Jaji Mkuu alipata wasaa wa kuzungumza na Mkuu
wa wilaya hiyo, Angelina Kwingwa ambaye alimshukuru Jaji Mkuu kwa
mkakati wa Mahakama wa kukarabati na kujenga majengo ya mahakama maeneo
mbalimbali nchini ambayo yatasaidia kupunguza mashauri mahakamani.
“Tumepata
faraja kusikia suala la kuongezeka kwa majengo ambayo yatasaidia
kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani na upatikanaji wa haki kwa
wakati”, alisema.
Jaji
Mkuu anaendelea na ziara Mahakama kuu kanda ya Tabora inayojumuisha
mikoa ya Tabora na Kigoma. Leo alitembelea na kukagua shughuli za
Mahakama katika Mahakama ya Mwanzo Ilolangulu, Mahakama ya wilaya ya
Urambo na Mahakama ya Mwanzo Upuge-Uyui zilizopo mkoani Tabora.
chanzo:Mpekuzi.
Comments