Rais Omar Hassan al Bashir ametangaza kuwa hana hamu ya kuwa mgombea katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2020 huko Sudan na atamuunga mkono shakhsia yoyote atakayechaguliwa na wananchi.
Rais Omar al Bashir aidha ametahadharisha kuhusu jitihada kubwa zinazofanywa na maadui wa Sudan za kutekeleza mashambulizi ya kisiasa na kiuchumi dhidi ya nchi hiyo na kueleza kuwa maadui wameendelea kubadili mbinu zao za kutoa pigo kwa Sudan.
Amesema maadui hao mara hutumia njia ya mashambulizi ya kijeshi na wakati mwingine njia ya udiplomasia na vile vile kupitia Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Sudan.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni makundi yanayomuunga mkono Rais Omar al Bashir yalimtaka agombee tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu. H
ata hivyo katiba ya Sudan hairuhusu kutekelezwa jambo hilo na kwa mujibu wa sheria za ndani za chama chake, Rais al Bashir haruhusiwi kugombea kwa mara nyingine.
Omar al Bashir amekuwa katika hatamu za uongozi nchini Sudan tangu mwaka 1989 kufuatia kutofanyika uchaguzi au kukosekana mpinzani anayewezeka kuchuana naye katika uchaguzi.
Rais wa Sudan anasakwa kimataifa akituhumiwa kutenda jinai za kivita na dhidi ya binadamu katika mapigano yaliyojiri katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan na kusabababisha vifo vya watu laki mbili.
chanzo:parstoday.
Comments