Mwili wa Akwilina Wawasili Kiijijini Kwao Rombo kwa Mazishi....Viongozi mbalimbali wameanza kuwasili.
Viongozi
mbalimbali wa Serikali wameanza kuwasili nyumbani kwa wazazi wa
aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina
Akwilini kijiji cha Marangu, Kata ya Marangu Kitowo, Olele mkoani
Kilimanjaro.
Mwili
wa mwanafunzi huyo aliyeagwa jana katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini
Dar es Salaam umefika kijijini hapa leo Februari 23, 2018 saa 3:30
asubuhi.
Viongozi
waliofika mpaka sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Leonard
Akwilapo, Mkuu wa Chuo Cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na
viongozi wengine wa wilaya.
Ibada
ya misa ya kuombea mwili wa marehemu inatarajiwa kuanza saa 6:00 mchana
katika kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele.
chanzo:mpekuzi.
Comments