Mkuu wa Wilaya ampongeza Mumewe kwa Kuongeza Mke.

Inawezekana ikaonekana ajabu kwa wengi kutokana na ugumu wa Wanawake wengi kukubaliana na sheria ya Dini ya Kiislam ya mume kuruhusiwa kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini hilo limekuwa jepesi kwa mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah baada ya kumruhusu, kumuandaa na kumpongeza mumewe kwa kuengeza mke wa pili.
Bi. Zainab Abdallah ambaye anatajwa kama Mkuu wa Wilaya Mdogo kabisa kwasasa hapa Tanzania ni Mke halali wa Abdul Muhammed ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam nawalifunga ndoa takribani miezi 7 iliyopita.
Mkuu wa wilaya huyo amezitoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram kwa kuandika na kuweka picha ya Bi Harusi na Mumewe baada ya kufunga ndoa.
Assalaam Alaykum,
Nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu @vanmohamed kwa kuongeza Mke wa Pili. Kwa kuwa dini yetu ya kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi.

Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu @only_chibeb wa kusaidiana nae majukumu mazito ya ulezi wa mume.
Alhamdulillah, M/Mungu ametupa rizki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.

Karibu sana kwenye familia @only_chibeb nimekupokea kwa mikono miwili na inshaaAllah M/Mungu atupe maskilizano na tuishi na mume wetu kwa wema till Jannah InshaaAllah.
Baaraka llahu lakumaa, wabaraka alaykumaa, wajamaa baynakumaa fil khaeyr❤❤🙏🏼
Abdul Mohammed akiwa na Mke mdogo baada ya kufunga ndoa

Comments