Mkuu wa propaganda wa al Qaida kaskazini mwa Afrika, auawa.

Mkuu wa propaganda wa al Qaida kaskazini mwa Afrika, auawaWizara ya Ulinzi ya Algeria imetangaza habari ya kuangamizwa magaidi wanne akiwemo mkuu wa propaganda wa mtandao wa al Qaida, kaskazini mwa Afrika.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, askari wa Algeria wamefanikiwa kuangamiza magaidi wawili akiwemo Hisham Abu Rawaha, mkuu wa propaganda wa mtandao wa al Qaida kaskazini mwa Afrika, katika operesheni iliyofanywa na askari hao kwenye eneo lililoko umbali wa kilomita 400 mashariki mwa  mji mkuu, Algiers. Magaidi hao hatari walikuwa wanasakwa na askari wa Algeria tangu mwaka 1994.

Magaidi wengine wawili wameangamizwa na jeshi la Algeria katika wilaya ya al Madiyah lililloko umbali wa kilomita 80 kusini mwa mji mkuu Algiers.

Siku ya Ijumaa pia wizara hiyo ya ulinzi ya Algeria ilitangaza habari ya kuangamizwa magaidi wanane hatari wakiwemo viongozi kadhaa wa mtandao wa al Qaida katika mkoa wa Khinlash.

Nchi nyingi zinazopakana na Algeria kama vile Libya, Mali na Niger hazina hali nzuri ya kiusalama hasa kutokana na kuripotiwa hivi karibuni kwamba baadhi ya makundi ya kigaidi yameligeuza eneo la kaskazini mwa Afrika kuwa kambi yao kuu baada ya kushindwa katika nchi kama za Iraq na Syria.
 
chanzo: parstoday.

Comments