
Hayo wameyaeleza wananchi hao huko Chuo cha Amali Mkokotoni wakati walipokuwa wakipatiwa Elimu ya Sheria ya Ardhi na kupiga vita aina zote za udhalilishaji zilizopo katika shehiya zao.
Wanachi hao wamesema wamechoshwa na vitendo na vitendo vya udhalilishaji na migogoro ya Ardhi ambayo hujitokeza sikuhadisiku katika shehiya zao jambo ambalo linarudisha nyuma kimaendeleo.
Aidha wamesema ni vyema Mawakili hao kuwa mstari wa mbele katika kusimamia sheria za Wananchi hao ili kuhakikisha vitendo hivyo vinaondoka Nchini.
“Tumechishwa na vitendo hivyo simamieni Sheria tuondowe kabisa katika nchi yetu”,Walisisitiza Wananchi hao.
Nao Mawakili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamesema wataendelea kutoa elimu kwa Wananchi mbali mbali wa Vijijini ili kuzifahamu na kuzitekeleza vyema Sheria hizo.
Hata hivyo Mawakili hao wamewataka Wananchi hao kuzifahamu ipasavyo Sheria ya Ardhi na Sheria ya Mahakama ya Kadhi ili kuwawezesha kuepukana na migogoro isiyokuwa ya lazima katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha wamesema wameamuwa kupita maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwapatia elimu wananchi hao katika kumiliki Ardhi kisheria na kupiga vita aina zote za udhalilishaji zilizopo katika shehiya zao.
Mawakili hao wamesema kutokana na sheria zilizowekwa katika Mahkama hiyo Mtu yeyote atakae miliki Ardhi ni vyema kujisajili ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima ndani ya Serikali na jamii kwa ujumla.
Ali Issa Abdalla mmoja ya Mawakili alisema wamechoshwa na vitendo vya udhalilishaji wanavyovisikia siku hadi siku vikiendelea ndani ya jamii jambo ambalo linalowaumiza vichwa katika utekelezaji wamajukumu yao.
Alisema licha ya Vitendo hivyo kuripotiwa siku hadi siku lakini wananchi walio wengi bado hawajawa na utayari wa kwenda kutoa ushahidi mahakamani kama inavyotakiwa.
“Utafiti ulibainisha ya kwamba Sheria iliyofutwa ilikuwa na mapungufu kadhaa ambayo bila ya kuondolewa udhalilishaji wa kijinsia ungelibakia kupigiwa kelele za bure na utekelezaji wa haki katika Mahakama za Kadhi ungeendelea kusuwasuwa” Alisema Wakili huyo.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na Watoto wao na kufuatilia nyenendo zao ili kuondokana na matatizo yanayowakabili watoto hao.





chanzo:Zanzibar24.
Comments