Marekani yampendekeza anayewachukia Waislamu kusimamia idara ya wahamiaji UN.

Marekani yampendekeza anayewachukia Waislamu kusimamia idara ya wahamiaji UNUtawala wa Rais Donald Trump wa Marekani umependekeza mtu anayewachukia Waislamu na mwenye misimamo mikali ya Kikrsito kusimamia Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji IOM.

Taarifa zinasema Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imempendekeza Ken Issacs, naibu mwenyekiti wa shirika la Kikristo la kutoa misaada linalojulikana kama Samaritan's Purse (Mfuko wa Wasamaria) kusimamia shirika hilo lenya bajeti ya mamilioni ya dola na ambalo huhusika na kuwasaidia wakimbizi kote duniani. 
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, Issacs amewahi kutoka matamshi ya kuwatusi na kuwavunjia heshima Waislamu katika mitandao ya kijamii na mahojiano ya radio.
Marekani ambayo ni kati ya wafadhili wakubwa wa IOM inashinikiza Issacs awe mkuu wa shirika hilo ambalo lina bajeti ya tarkibani dola bilioni moja kwa mwaka na lenye nchi wanachama 169.
Kuna wasiwasi kuwa, afisa huyo aliyeteuliwa na Marekani huenda akashindwa vibaya katika upigaji kura miongoni mwa nchi wanachama na hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Marekani kudhalilishwa katika upigaji kura huo tokea muongo wa 60.
Mwezi Desemba mwaka jana Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein alikosoa hatua ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump aliyesambaza taswira zilizo na chuki dhidi ya Uislamu kupitia akaunti yake ya Twitter.
Katika taarifa yake, Al Hussein amesema, hatua ya Trump ya kupokea na kusambaza taswira kadhaa zilizo dhidi ya Waislamu ni jambo lenye kuzusha uchochezi.
Chuki za Trump na utawala wake dhidi ya Uislamu na Waislamu si jambo jipya wala geni. Mwaka 2015, na kabla ya kujitosa kwenye kampeni za kuwania urais wa Marekani, alidai kuwa "Uislamu unaichukia Marekani."
 Wakati wa kampeni za uchaguzi Trump aliahidi kuwa endapo angeshinda na kuingia Ikulu ya White House angewazuia Waislamu kuingia nchini Marekani, na kivitendo ndivyo anavyofanya sasa.
 chanzo:parstoday

Comments