Ili kufikia lengo hilo Marekani imeendesha harakati zake katika ngazi ya kieneo kwa kushirikiana na Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel.
Aidha katika uwanja huo, tarehe 13 Oktoba mwaka jana Marekani iliandaa stratijia ya kiuhasama dhidi ya Tehran, sambamba na kuanza kutekeleza hatua kadhaa kupitia fremu ya kile ilichosema kuwa ni vitisho vya kiusalama kutoka kwa Iran.
Kuharibu makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, kuwekwa vikwazo vipya na kueneza propaganda kwamba uwezo wa kiulinzi wa makombora ya Iran ni hatari, ni mihimili mitatu ambayo inaunda stratijia za kiuhasama za Washington dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kuhusiana na suala hilo Jumamosi iliyopita, Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine sambamba na kusisitiza juu ya haki isiyopingika ya Jamhuri ya Kiislamu katika kutetea maslahi yake ya kitaifa na kulinda usalama wake wa taifa, alisema:
"Iran kwa uwezo wake wote, itaendelea kufuatilia mipango, malengo na stratijia za kiulinzi hususan katika uwanja wa uwezo wake wa makombora."
Kwa hakika serikali ya Trump imefanya makosa mengi katika stratijia zake, hata hivyo kile ambacho kinashuhudiwa ni kwamba Washington hadi sasa bado inaendelea kufanya makosa hayo.
Ili kufikia malengo yake ya kishetani, Rais Donald Trump ameunda ushirikiano wa pande tatu, yaani Marekani, Saudia na utawala haramu wa Kizayuni kwa ajili ya kutekeleza hatua haribifu dhidi ya Iran ya Kiislamu.
Kuhusiana na suala hilo Vladimir Sagien, mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa Russia anasema: "Hadi sasa Marekani bado inakabiliwa na tatizo la kuionyesha Iran kuwa ni tishio, suala ambalo linachochewa zaidi na Saudia na Israel." Mwisho wa kunukuu.
Katika uwanja huo Washington inafanya kila hatua ili iweze kufikia malengo yake hayo.
Miongoni mwa hatua mpya kabisa za Washington ni kuliweka jina la Ismail Haniyah, Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika orodha eti ya magaidi.
Hata hivyo ni vyema kufahamu kwamba, orodha hiyo inayotajwa kuwa ya ugaidi na Marekani, kwa hakika ni orodha ya wapinzani wa siasa za kiuhasama na zilizo dhidi ya binaadamu za Washington au wale wanaopambana na wavamizi wa Kizayuni wanaotenda jinai kila uchao dhidi ya Wapalestina.
Harakati kama hizo pia zinatekelezwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi ambazo zinapinga siasa zake za kimabavu. Katika hilo hivi karibuni Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia, katika safari zake za kila mara barani Ulaya anajaribu kuzihonga kwa dola za mafuta baadhi ya nchi za bara hilo ili ziweze kuchukua hatua kali dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ni kwa ajili hiyo ndio maana hivi karibuni Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba:
"Kadri Trump na washirika wake watakavyopiga tarumbeta za propaganda kwa lengo la kupindisha ukweli wa mambo na kadri Saudia itakavyoendesha propaganda zake chafu, hawataweza kubadilisha ukweli wa mambo."
Ukweli ni kwamba, Marekani, Saudia na Israel ziko kwenye mkwamo wa kisiasa.
Kuhusiana na suala hilo, Sadiq Kushki, mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa nchini Iran anasema:
"Kwa kuanzisha mahusiano na utawala wa Kizayuni, watawala wa Saudia watatengwa na ulimwengu wa Kiislamu. Si tu kwamba Saudia haina mahusiano mazuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pekee, bali Wasaudi wameshindwa kufanya mahusiano mema na nchi nyingine za eneo la Mashariki ya Kati kama vile, Iraq, Uturuki na Qatar."
Mwisho wa kunukuu. Marekani, Saudia na Israel zinafanya njama mtawalia katika uga wa kimataifa dhidi ya Iran kwa kuitaja nchi hii kuwa tishio, hata hivyo mataifa ya eneo na dunia kwa ujumla inafahamu kwamba muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudia na kuungwa mkono na Marekani na Israel, ndio unaotumia silaha nyingi ulizozipata kutoka kwa madola ya Magharibi kutekeleza mauaji ya maelfu ya wanawake na watoto wa Yemen na kuwafanya zaidi ya milioni saba kuwa wakimbizi.
chanzo:parstoday.
Comments