
Amesema viongozi wana nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika kuwaelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo kwani upinzani sio chuki na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya uraia hasa kwa vijana.
Hata hivyo Juma Ali Khatibu amewataka viongozi kukumbuka na kuwacha kujisahau wakati wanapochaguliwa kupewa madaraka ya uongozi na wananchi kwani bila ya kuchaguliwa na kuaminiwa wasingekuwa na vyeo walivyonavyo hivi sasa.
Aidha ametoa wito kwa baadhi ya viongozi wanaoshindwa kutimiza majukumu yao kwa wananchi waliowachagua kuwajibika ipasavyo kwani wao ni watetezi hasa kwa wananchi wanyonge kusikiliza vilio na changamoto zinazowakabili wananchi.
chanzo:Zanzibar24
Comments