KIPA wa Yanga, Youthe Rostand, amethibitisha kuendelea vizuri akirejea sasa katika ukakamavu huku akiwa ameshaanza kufanya mazoezi na wenzake na kusema siku chache zijazo mashabiki watamuona uwanjani.
Rostand aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli mwezi huu, hivyo kuliacha lango la timu hiyo kwa chipukizi, Ramadhani Kabwili ambaye hata hivyo anafanya vizuri.
Kipa huyo raia wa Cameroon ameliambia Mwanaspoti alikaa nje baada ya kuambiwa apumzike na daktari, lakini sasa anafanya mazoezi na wenzake.
“Nimeshaanza mazoezi, lakini nimeambiwa niwe napumzika ili niwe fiti zaidi na kuitumikia timu yangu katika mashindano,” alisema.
“Unajua unapotoka benchi la majeruhi inahitaji upate muda wa kurejea taratibu usije ukaumia zaidi.
“Sina tatizo lingine lolote zaidi ya lile la majeruhi, kukosekana kwangu katika mechi za kimataifa ni kwa sababu naumwa, ndio maana hata katika mechi za ligi pia nimekosekana.”
chanzo:Mwanasport.
Comments