Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabili liyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando hadi February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Mwendesha
Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea Tido
maelezo ya awali.
Hata
hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa
amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya
(Ph), hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Inadaiwa
alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC
alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa
vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza
zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.
Inadaiwa
kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu, kama
muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake
alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.
chanzo:Mpekuzi.
Comments