Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu na kitaifa yataka kuona matokeo ya fursa za masoko katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Akiwasilisha ripoti hiyo ya kamati katika kikao cha baraza la wawakilishi Mwenyekiti wa kamati ya kusimami ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa Omar Seif Abeid amesema pia idara lazima iwe inatoa taarifa za mpango wa kupunguza umaskini ili jamii iweze kuelewa hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuondoa umaskini nchni.
Wakati huo huo Mwenyekiti huyo wa kamati ya kusimamia Ofisi za viongozi amezungumzia changamoto zinazoikabili tume ya kitaifa ya uratibu na udhibiti dawa za kulevya nchini ambapo amezitaja miongoni mwa changamoto hizo ni upotevu wa vielelezo vya kesi na kukosekana kwa takwimu halisi juu ya idadi ya vijana walioingia na kutoka katika vituo vya tiba na Marekebisho ya tabia sober house.
Baada ya kugudnua changamoto hizo Kamati hiyo imetoa ushauri kwa tume ya uratibu na udhibiti wa dawa za kulevya kuwa karibu na taasisi zote zinazohusika na kesi za madawa ya kulevya ili kuhakikisha kwamba wale wote wanaojishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya wanachukuliwa hatua za kisheria na kwamba tatizo la upotevu wa vielelezo vya kesi hizo halitokei tena kama hapo awali.
Comments