Utawala wa Kizayuni wa Israel umepatwa na kiwewe baada ya ndege yake ya kisasa ya kivita aina ya F 16 kutunguliwa na jeshi la anga la Syria, na hivyo kutoa madai hayo yasiyo na msingi kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imehusika katika shambulizi hilo.
Israel imedai kwamba, ndege zake kadhaa ziliifuatilia ndege isiyo na rubani ya Iran ambayo ilivuka anga ya Syria na kuingia Israel ambapo baadaye ilitunguliwa na jeshi la utawala huo na baada ya hapo kuzishambulia taasisi za Iran zilizoko nchini Syria.
Kufuatia madai hayo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amekadhibisha taarifa ya ndege isiyo na rubani ya Iran iliyopaa katika anga ya Israel na kadhalika kuhusika Tehran katika kuangamizwa ndege ya kivita ya utawala huo haramu wa Israel na kwamba madai hao ni dhihaka na kichekesho kikubwa.
Bahram Qassemi ameongeza kwamba, Iran ya Kiislamu ipo nchini Syria kama mshauri baada ya kuombwa rasmi na serikali ya Damscus.
Kadhalika ameashiria uvamizi wa hivi karibuni wa ndege za kivita za utawala haramu wa Israel nchini Syria na kubainisha kwamba,
Syria kama taifa lenye kujitegemea inayo haki ya kulinda ardhi yake yote na kukabiliana na kila aina ya uvamizi wa Israel.
Pia ameitahadharisha Tel Aviv kwamba, kamwe haitaweza kujisafisha kupitia kubuni uongo na upotoshaji wa jinai na ukatili wa kila mara unaoufanya dhidi ya mataifa ya Waislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla.
chanzo:parstoday.
Comments