Helikopta ya kijeshi yaanguka Tunisia na kuua na kujeruhiwa wanajeshi.

Helikopta ya kijeshi yaanguka Tunisia na kuua na kujeruhiwa wanajeshiMsemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Tunisia ametangaza habari ya kuanguka helikopta moja ya kijeshi ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na kuua mwanajeshi mmoja na kujeruhi wengine wawili.

Shirika la habari la al Jazeera limemnukuu Kepteni Belhasn al Waslati akithibitisha habari hiyo na kusema kuwa helikopta hiyo imeanguka muda mchache baada ya kuruka katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa mji wa bandari wa Sousse, nchini Tunisia na kuua mwanajeshi mmoja na kujeruhi wengine wawili. 
Kwa mujibu wa msemaji huyo, hali ya majeruhi ni mbaya na wamelazwa katika hispitali ya kijeshi mjini Tunis. Mwanajeshi aliyekufa, amepoteza maisha akiwa hospitalini.
Sami er Refik, daktari katika hospitali waliyolazwa wanajeshi hao amesema hali ya majeruhi waliobakia nayo ni mahututi.
Hata hivyo hakukutolewa maelezo zaidi kuhusu sababu za kuanguka helikopta hiyo ya kijeshi. 
Mwezi Julai mwaka jana pia, helikopta moja ya kijeshi ilianguka katika mji wa Sfax wa katikati mwa Tunisia na kuua rubani na abiria mmoja. 
msaemaji wa jeshi la Tunisia, Kepteni Belhasan al Waslati alithibitisha habari hiyo na kusema kuwa helikopta hiyo ilikuwa ya kutolea mafunzo kwa wanajeshi na ilianguka na kuua wanajeshi wote wawili waliokuwemo ndani yake.
chanzo:parstoday.

Comments