Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Angelina Mabula amesema ni
marufuku halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa
fidia.
Mhe.
Mabula amesema hayo Wilayani Butiama mkoa Mara wakati wa ziara yake
yenye nia ya kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa
ukusanyaji kodi ya ardhi.
Amesema
wakati wa mchakato wa kuchukua maeneo ya mwananchi ni vyema wahusika
wakashirikishwa kuanzia hatua ya awali sambambana na kuelimishwa juu ya
zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.
‘’Cha
msingi ni kuanza kuzungumza na mwananchi kabla ya kuchukua eneo lake na
kumueleza eneo ambalo ataachiwa na halmashauri zihakikishe mwananchi
huyo anapimiwa pamoja na kupatiwa hati yake’’ alisema Mabula
Aidha,
mhe. Mabula amesema eneo litakalochukuliwa na halmashauri viwanja vyake
kuuzwa fedha itakayopatikana halmashauri ihakikishe inatumika katika
kutengeneza miundo mbinu na huduma nyingine za jamii na kusisitiza kuwa
kwa kufanya hivyo migogoro haiwezi kutokea.
Naibu
waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ameziagiza halmashauri
kuhakikisha zinapanga miji kulingana na ‘master plan’ ili kuwa miji bora
iliyopangika
chanzo:Mpekuzi.
Comments