
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Sita wa chama cha walimu Zanzibar zatu amesema serikali imeamua kuondoa ada kwa wanafunzi kwa lengo la kuendeleza sera ya rais wa awamu ya kwanza Shekh Abeid Amani Karume.
Amesema sera ya elimu bure itaimarika endapo walimu watafanya kazi kwa mujibu wa sheria na maendeleo ya elimu yatajengeka iwapo walimu watakuwa na juhudi na uimara pamoja na misingi bora na zamira njema ya kufundisha wanafunzi maskulini.
Dr. shein amesema anatambua matatizo yanayowakabili walimu pamoja na skuli kukabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo uhaba wa walimu, uchache wa vifaa vya kufundishia pamoja na malimbikizo ya madeni ya mishahara ya walimu na kuiagiza wizara ya elimu kuhakikisha wanawalipa madeni yote wanayodaiwa na walimu kabla ya kufikia 2019 kwani kuendelea deni hilo litaweza kuondoa ari ya walimu kufundisha na kupelekea sekta ya elimu kuyumba kutokana na maslahi madogo ya walimu.
Hata hivyo Rais Shein amesema amerizishwa na matokeo yaliyopatikana katika mitihani ya taifa kwa elimu ya msingi na sekondari na kuitaka wizara ya elimu kukaa pamoja na skuli zote za Zanzibar zile zilizofanya vibaya katika mitihani ya taifa ili kuweza kujua sababu zilizopelekea kufeli.
Aidha amesema serikali itaendelea kujali na kuthamini michango ya walimu yanayotoka katika taifa kwa kujali maslahi yao kila uchumi wan chi utakavyo imarika.
Kwaupande wake Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar zatu Mussa Omar Tafurwa Mapema akisoma risala ya walimu amesema miongoni mwa matatizo yanayowakabili ni tatizo la uhaba wa walimu kwa skuli za pemba na mikoa ya kaskazini na kusini kwa unguja.
Tafurwa ameiyomba serikali kufanya uwekezaji wa rasilimali fedha ya kutosha ili kuweza kuajiri walimu pamoja,kununulia vifaa vya kufundishia pamoja na kulipa madeni ya walimu wanayodai kwani pia baadhi yao wamesha staafu na wengine kufariki.
Amesema pia licha ya matatizo hayo pia walimu wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufundishia ambapo hupelekea kuumwa na kushindwa kufanya kazi vizuri hivyo wameiyomba serikali kuwaanzishia bima ya afya kwani wanashindwa mukumu gharama za matibabu kwani fedha wanayoipata bado haikidhi haja.
chanzo:zanzibar24.
Comments