Mwanamme mmoja alietambulika kwajina la Is-haka Ibrahim Abdallah
mwenye umri wa miaka 36 amshushia kipigo kizito mkewe na kummwagia
mafuta yataa kwa lengo la kumripua na hatimae kukimbilia nyumbani kwa
sheha na kupata msaada.
Tukio hilo limetokea saa moja na nusu usiku huko Kibweni Wilaya ya Magharib A Unguja.
Majeruhi huyo akielezakwa masikitiko mkasa huo ulivyotokea amesema “kuwa
nilikua namuaga kuwa naendazangu nyumbani kwa hali yangu akainuka na
kuanza kunipiga na akachukua kisu akataka kunichania nguo amenipiga na
kuniumiza na aliniambia anataka kunichoma kisu pia aliniambia
atakaponikuta popote atanipiga amenipiga nimevimba mwilini amenichuna na
baada ya hapo alikuja na mafuta ya taa akanimwagia ili anichome moto”
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Sheha wa Shehia ya Kibweni Subira Haji Yahya anaeleza mkasa huo “kesi
hii imetokea kweli mama huyo amekuja nyumbani mwangu nakilio na nguo
zake zime chanika sehemu za mwili zilikua zipo wazi nayeye alipokuja
alisema kweli alikua anataka kumchoma moto”
Hadi sasa kesi hiyo imeshafikishwa Kituo cha Polisi Bububu.
chanzo: zanzibar24.
Comments