Cyril Ramaphosa alisema hayo jana na kuongeza kuwa, tayari ameanza mazungumzo na Rais Jacob Zuma kuhusiana na suala la kukabidhi madaraka na masuala mengineyo.
Ameongeza kuwa, matokeo ya mazungumzo yao yatajulikana siku chache zijazo na wakati huo ndipo itajulikana hatima ya Rais Jacob Zuma.
Ramaphosa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Afrika Kusini amesema, mazungumzo yake na Jacob Zuma yalikuwa mazuri na yamechunguza njia bora na za haraka za kutatua matatizo ya nchi hiyo.
Rais Jacob Zuma amezidi kuwa chini ya mashinikizo ya chama tawala cha ANC tangu Cyril Ramaphosa alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Hivi sasa ANC imegawika baina ya waungaji mkono wa Zuma na wapinzani wake na hadi sasa imeshindwa kumlazimisha Jacob Zuma ajiuzulu kabla ya kumalizika kipindi chake cha urais mwakani.
Iwapo Jacob Zuma atajiuzulu, Cyril Ramaphosa ambaye ni makamu wake atachukua uongozi wa Afrika Kusini hadi utakapoitishwa uchaguzi mwingine wa rais mwaka 2019.
Comments