Uongozi wa klabu ya Yanga unatoa taarifa kwa umma kuwa siku
ya Jumapili Januari 7, 2018 kwenye uwanja wa Karume kutafanyika usaili
wa kusaka vijana wenye vipaji vya kusakata kabumbu.
Wazazi mnaalikwa kuleta vijana wenu ambao wako chini ya umri wa miaka 15.
Usaili huo utaendeshwa na wakongwe waliowahi kutamba kwenye kikosi
cha Yanga ambao ni Keneth Mkapa, Maalim Saleh, Edibily Lunyamila na
Ramadhani Kampila.
Comments