
Msaidizi wa Waziri Mkuu
amesema kuwa tafsiri isiyo sahihi ilipelekea yeye kunukuliwa visivyo
kwa kusema kuwa analenga kutoa fursa ya kuwepo kwa mashauriano ya
kisiasa.
Waziri Mkuu huyo pia alisema kuwa kituo kipya cha kuwazuilia wafungwa kitafungwa.
Awali
shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International lilipokea
habari hizo kwa kusema ni ishara ya "hatua ambayo huenda ikaachilia sura
mpya kwa haki za kibinadamu Ethiopia."
Japo pia lilionya kuwa
tendo la kufungwa kwa kituo cha kuwazuilia wafungwa cha Maekelawi
haliwezi 'kufuta vitendo vya ukatili' vilivyotokea katika jengo hilo.
Ethiopia
kwa muda mrefu imetuhumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu kwa
kuwakamata wapinzani wake kwa wingi na kuwazuilia katika juhudi za
kuzima upinzani dhidi ya serikali.
Hata hivyo, hii ndiyo mara ya kwanza kwa serikali kukiri kwamba inawazuilia wafungwa wa kisiasa.
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema awali serikali imekuwa ikiwaita "wahalifu".
Haijulikani wafungwa hao ni wangapi na wataachiliwa huru lini.
Shirika
la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limekuwa
likiituhumu serikali kwa kutumia sheria za kukabiliana na ugaidi
kuwafunga wapinzani wake.
Wanaozuiliwa
katika magereza na vituo mbalimbali kote nchini humo ni pamoja na
wanaharakati wa upinzani kutoka majimbo ya Amhara na Oromia.
Majimbo hayo yalishuhudia maandamano ya kupinga serikali 2015 na 2016.
Kuna piawatu kutoka jimbo la watu wa mataifa ya kusini, na wanahabari ambao wamekuwa wakiikosoa serikali.
Ni
vigumu kueleza hasa ni wafungwa wangapi wa kisiasa wanazuiliwa nchini
humo, lakini mwandishi wetu anakadiria kwamba kuna takriban watu 1,000
wanaozuiliwa kwa makosa mbalimbali chini ya sheria za kupambana na
ugaidi.
Kuna wengine 5,000 ambao kesi zao bado zinasikizwa, wengi ambao walikamatwa wakati wa hali ya hatari Oktoba 2016.
Serikali haijaeleza wataachiliwa lini au ni nani hasa wataachiliwa.
Kuna waliofungwa kwa sababu za kisiasa lakini kunao waliofungwa wakihusishwa na ugaidi.
Watu 19 waliohusishwa na kundi la Ginbot 7 linalochukuliwa na serikali kuwa kundi la kigaidi walifungwa jela wiki hii.
Bw
Hailemariam amesema kituo kikuu cha kuwazuilia wafungwa cha Maekelawi
mjini Addis Ababa ambacho HRW tangu 2013 walidai kimekuwa kikitumia
mateso kupata habari kutoka kwa washukiwa kitafungwa.
Serikali imesema kitageuzwa na kuwa makumbusho ya kisasa.
Kituo kipya cha kuwazuilia washukiwa kitafunguliwa na Bw Hailemariam amesema kitatimiza viwango vya kimataifa.

chanzo:bbc.
Comments