
Gari hilo lilikuwa linasafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga
- Daktari mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu
Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki
amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece
ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama
kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na utingo wake
ni miongoni mwa waliofarikiBw Kayuki amesema hiece hiyo ilikuwa ikitokea
kibondo kwenda kahama ambapo malori yaliyohusika kwenye ajali hiyo
yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidiKamanda wa
jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha
taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya
waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa zitatolewa kwa umma bila
kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa
uhakika.
chanzo:Bbc.
Comments