
Watoto hao wametua na kupokewa na kituo cha Association For
Termination of Female Genital Multilation (ATFGM Masanga) Kufuatia hatua
hiyo, Serikali imewataka wazazi hao kutoa malezo ya kuwakataa watoto
wao baada ya kukataa kufanyiwa unyama huo kabla hawajachukuliwa hatua za
kisheria.
Akitoa agizo hilo kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious
Luoga, kaimu ofisa elimu msingi wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Amos
Waitara alivitaka vyombo husika vya Serikali kuhakikisha watoto hao
wanapata haki za malezi kutoka kwa wazazi wao.
Waitara alitoa agizo hilo wakati wa kufunga kambi ya wasichana 103
waliokuwa wamekimbilia katika kituo hicho na kupewa mafunzo mbadala
dhidi ya madhara ya ukeketaji na tohara.
“Hatuwezi kulifumbia macho suala hili kwa baadhi ya wazazi hawa
kuminya uhuru wa watoto walioona mbali na kuchukua jukumu la kupinga
vitendo vya kikatili vya ukeketaji, wazazi hao waitwe na kueleza kwa
maandishi sababu za kuwanyanyasa,” alisema .
Meneja miradi ATFGM, Valerian Mgani alisema tangu kituo hicho
kilipoanzishwa mwaka 2008 wamekuwa wakipokea watoto ambao wanakimbia
ukeketaji.
Wasichana hao hutoka wilaya za Serengeti, Tarime, Loliondo na nchi
jirani ya Kenya na kambi inapomalizika hurudishwa nyumbani na baadhi yao
wamekuwa wakikataliwa na wazazi.
Naomi Baraka kutoka nchi jirani ya Kenya ambaye alishiriki mafunzo
hayo ya tohara mbadala, aliiomba Serikali ya Kenya kuthamini watoto wa
kike huku akiitaka jamii kuondokana na mila ambazo zimepitwa na wakati.
Baadhi ya mabinti ambao hawakutaka kutaja majina yao kutoka kata za
Sirari, Pemba na Nyanungu wilayani Tarime waliolazimishwa kuolewa
katika umri mdogo na kukimbilia kituoni hapo waliiomba Serikali
kuingilia kati jambo hilo.
Kituo cha ATFGM Masanga mpaka sasa kina
mabinti 2,572.
Comments