Amesema kuwa sasa wamekusudia kufanya mabadiliko
makubwa katika sekta zote za huduma kwa wateja ili waweze kuwapa uzoefu
wa kukumbukwa wageni mbalimbali wanaokuja nchini pamoja na kutangaza
utamaduni wa nchi yetu.
“Ukarimu ni utamaduni wetu. Tunahitaji kuutumia
kibiashara. Lazima tubadilike, tuurejeshe kwa nguvu kubwa kwenye sekta
zote za huduma kwa wateja na tuutumie kuwapa wageni wetu ‘experiences’
nzuri za kukumbukwa waende wakatusemee kwa wenzao huko kwao, wakawe
mabalozi wetu. Tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye eneo hili”
Waziri aliendelea kusisitiza kuwa “Tanzania tuna wasichana warembo, kwa nini wasiajiriwe kwenye nafasi za kazi za ukarimu, tabasamu zao zikawa taswira ya wema na uungwana wetu kama Taifa! Tuna vijana imara, watanashati, wanaoweza kuwa taswira ya wema na uungwana wetu. Majirani zetu wametumia hii, Leo imekuwa taswira ya nchi zao wakati sisi tunawajua hawana uungwana wala wema hata chembe…wanetengeneza taswira bora ya nchi yao. Hii haitushindi. Tuelekee huko sasa” alisema Kigwangalla.
chanzo: zanzibar24.

Comments