
Maandamano yalizuka katika ukanda wa Gaza baada ya tangazo hilo.
Azimio
la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta tangazo hilo lake
liliunga mkono kwa wingi na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Wapalestina
13 wameuawa kwenye ghasia kufuatia tangazo hilo la Trump wengi wakiuawa
wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel.
Mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na wapalestina.
Israel
ilitwaa eneo la mashariki mwa mji, ambalo awali likuwa linakaliwa na
Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya masahariki ya kati na inadai
kuwa mji huo wote ni wake.
Leo Jumapili Bw Abbas aliutaja Jerusalem kuwa mji mkuu wa kiroho wa watu wa Palestina.
Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni hatua ambayo haijatambuliwa kimataifa, na nchi zote zimeweka balozi zao huko Tel Aviv.
Hata
hiyo Rais Trump ameiambia wizara ya mashauri ya nchi kigeni kuanza
mchakato wa kuhamisha ubalozi wa Marekani kwenda Jerusalem.
Wapalestina
wametangaza kuwa wamemuita balozi wao kutoka nchini Marekani kwa
mazungumzo, wiki kadhaa baada ya rais Donald Trump kutambua Jerusalem
kuwa mji mkuu wa Israel.
chanzo:Bbc.
Comments