Wananchi wa Kisiwa Panza Pemba wakumbushwa juu ya uhifadhi na udhibiti wa mazingiza.

Related imageNaibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Mazingira Pemba ( PEJO ) Nd. Marzouk Khamis  Sharif amesema kuwa iwapo jitihada za maksudi hazitochukuliwa kwa wananchi wa kijiji cha kisiwa panza Wilaya ya Mkoani katika suala zima la uhifadhi wa mazingira, bado athar za mabadiliko za tabia nchi zitaendelea kuathiri kutokana na ukataji mbaya wa miti iliyo zunguka kisiwa hicho.


Akizungumza na wananchi wa kisiwapanza marabaada ya kutembelea maeneo mbali mbali yakiwemo ya kilimo yaliyo athiriwa na maji chunvi ikiwa ni miongoni mwa jitihada za jumuiya hiyo kutoa elimu ya mazingira Nd. Marzouk amesema licha ya juhudi mbali mbali  zinazo chukuliwa namashirika binafsi, NGOs, na taasisi za Serekali lakini bado athar za mabadiliko ya tabia nchi zinaendelea kuathiri wananchi wa kisiwa hicho.


Amesema suala la uhifahdi wa mazingira nijukumu la kila mtu na sio taasisi moja tu, hivyo amewataka wananchi kupanda miti kwa wingi ili kuzuiya maji ya bahari yasivamie maeneo yakilimo.


Aidha Nd. MARZOUK amesema kitu cha msingi katika kuthibiti hali hiyo isiendelee ni kupanda miti ya mikandaa katika maeneo ya bahari, ili kuzuiya kasi ya maji kuingia mashambani.


Nae Mwajuma Ali Hassan ambae ni mkaazi wa Kisiwapanza amesema suala la ukataji wa miti ovyo limewaathiri sana wakulima kutokana na maeneo ya kilimo kuvamiwa na maji chunvi, ambapo zaidi ya eneo lenye ukubwa wa hekta 200 maeneo ya kilimo na makaazi ya wananchi yamesha athiriwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Comments